Sheria za Chesi

Hapa utapata kwa kiswahili sheria zote za mchezo wa chesi unazotakiwa kuzijua. Download the pdf here.

Mchezo nzuri!  

Kila mchezo utaanza kwa hatua kama iliyo hapo juu. Malengo ni kuwakamata maadui wa mfalme. Nyeupo siku zote anacheza wa kwanza, kisha anafuata nyeusi, kwa kila mchezo unaweza kusogeza kete moja (kasoro mruko). Kila kete inamwendo wake wa kipekee. Kete haiwezi kuhamia mraba wenye kete ya rangi yake, lakin ikimaliza mwendo wake kwenye mraba wenye kete yenye rangi nyingine inaikamata kete huyo.

Askari Pawn

Askari anasogea hatua moja kwa kila wakati, kasoro mbili: – Hatua ya kwanza anaweza kusogea mara moja au mbili – Askari hukamata kete iliyopo upande wa kushoto au kulia wa mraba mbele yake.

Askari

Farasi Knight

Ni kete pekee inayoweza kuruka juu ya kete nyingine, Farasi anachora mchoro wa L, anatembea hatua tatu mara zote. Hatua mbili mbele kila moja kulia au kushoto. Farasi anaenda mraba wenye rangi tofauti na aliyokua mwanza, kama alikua nyeupe, atakua nyeusi, na kama alikua nyeusi atakua nyeupe.

Farasi

Askofu– Bishop

Anatembea mshazari, askofu hawezi kubadilisha rangi, askari anaenda mshazari haraka awezavyo kwa viboksi visivyokua na kete nyingine.

Askofu

Ngome Rook

Anatembea kwenda mstari mnyoofu, anaenda kulia au kushoto, anaenda mbele au nyuma, miraba mingi awezavyo iliyopo wazi bila kete nyingine.

Ngome

Malkia Queen

Ni kete yenye nguvu kuliko zote katika mchezo wa chesi, anaweza kwenda nyuma, mbele, kulia, kushoto au mshazari, anaweza kwenda mbali miraba mingi iliyo wazi.

Malkia

Mfalme King

Ni kete ya muhimu zaidi katika mchezo wa chesi, kama atakamatwa basi utakua umepoteza mchezo. Mfalme anaweza kwenda kulia, kushoto, mbele au nyuma na hata mshazari, lakini anatembea hatua moja tuu.
Mfalme hawezi kusogea kwenye kiboski ambacho atakua kwenye hatari ya kukamatwa.

Mfalme

Kuogopesha kutishia– Check!

Maana ya check ni kete ya adui inaweza kumkamata mfalme, kama mpinzani anaweza kuitishia mfalme mshambuliwa ananjia tatu
–         Kula kete ambayo inasababisha tishio
–         Kukata tishio kwa kuweka kete nyingine mbele ya mfalme
–         Kuondoka katika mraba unao shambuliwa kwenda mahali pasipo shambuliwa

Mkwamo – Checkmate!!!

Kushinda. Ni kama mfalme hawezi kutoka katika tishio hiyo tunasema ni mkwamo.

Kukamata – Capturing

Ukisogeza kete yako hadi kwa adui, unatoa hapo kete ya adui kasha unaweka yako na ya adui inaenda nje.

Kuruka ngome – Castling

Kunamwendo mmoja wa pekee kama mfalme na ngome hazikutembea bado na kete zote zilizopo kati yao zimeshaondoka. Hapa mfalme anaruka miraba miliwi kwelekea ngome na ngome inaruka upande mwingine wa mfalme.
Masharti ya mwendo huu ni:
–         Mfalme wala ngome hazikusogea bado
–         Hakuna kete kati yao
–         Mfalme hashambuliwi moja kwa moja
–         Mraba itakapofikia mfalme haitishiwi wakati wa kuruka

Kukamata kwa kupita  – En passant

Kama utasogeza askari miraba miwili, askari wa adui anaweza kuikamata kama lisogea mraba mmoha, mara baada ya wakati mwingine.

Droo – Draw

Kama hakuna mchezaji anaweza kushinda hiyo ni droo.

Kujinyonga – Stalemate

Kama mfalme hajashambuliwa, na kwa hatua yoyote atakayoifanya atashambuliwa basi mfalme atakua amejinyonga na hi ni droo. 

Imeandikwa na Mwalimu I. Silayo

Leave a comment